Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vodacom yatangaza mkurugenzi mtendaji

Wed, 27 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baada ya takriban miezi sita, bodi ya wakurugenzi Vodacom imemthibitisha Hisham Hendi kuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo kubwa ya mawasiliano nchini.

Hendi aliteuliwa kukaimu nafasi hiyo Septemba Mosi mwaka jana na kwa mujibu wa taarifa ya mwenyekiti wa bodi ya Vodacom, Ali Mufuruki atakuwa mkurugenzi mtendaji kuanzia Machi 19.

“Hendi ana uzoefu wa miaka 15 katika sekta ya mawasiliano na amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi katika nchi za Ulaya, Misri na Afrika Kusini. Tuna imani chini ya uongozi wake, Vodacom itaendelea kutoa mchango katika jamii na kuisaidia Tanzania kufikia malengo ya maendeleo,” amesema Mufuruki.

Hendi alishika wa ukaimu baada ya aliyetarajiwa kuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo, Sylivia Muringe kutoka Kenya kukosa vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini.

Sylivia ilikuwa arithi mikoba iliyoachwa na Ian Ferrao aliyeiongoza Vodacom kwa miaka mitatu kabla hajaamua kustaafu kwa hiyari ili akafanye mambo mengine.

Ingawa inaongoza kwa gharama kubwa za kupiga simu au kutuma ujumbe mfupi  ndani ya mtandao, Vodacom ndio mtandao unaohudumia wateja wengi zaidi nchini.

Takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ya robo ya mwisho mwaka jana inaonyesha wateja wa Vodacom walikuwa wanalipa Sh270 kupiga simu kwa kila dakika moja ikilinganishwa na Sh60 waliyokuwa wanalipa wateja wa Benson au Sh154 ya wale wa TTCL. Ujumbe mfupi ulitozwa Sh51 wakati Halotel wakilipa Sh30 na Benson Sh40.

Hata hivyo, Vodacom ilikuwa na wateja milioni 14.14 kati ya milioni 43.62 waliokuwa wamesajiliwa mpaka kipindi hicho wakati Smart ikiwa nao 132,292 tu. Vodacom pia inaongoza kwa wateja wengi wa huduma za fedha, mpaka Desemba, M-Pesa ilikuwa na wateja milioni tisa wakilinganishwa na 30,394 wa TTCL Pesa.



Chanzo: mwananchi.co.tz