Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vodacom yaridhishwa ongezeko umiliki soko

HISHAM Vodacom yaridhishwa ongezeko umiliki soko

Tue, 12 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom, imetoa matokeo ya awali ya kifedha kwa mwaka, unaoishia Machi 31, mwaka huu, ikionyesha ukuaji wa kibiashara unaodhihirishwa na ongezeko la umiliki wake wa soko kufikia asilimia 32.8.

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom, imetoa matokeo ya awali ya kifedha kwa mwaka, unaoishia Machi 31, mwaka huu, ikionyesha ukuaji wa kibiashara unaodhihirishwa na ongezeko la umiliki wake wa soko kufikia asilimia 32.8.

Mafanikio hayo yametokana na kuongeza idadi ya wateja wake wapya milioni 1.4 na kufikisha jumla ya wateja milioni 15.5.

Hayo yalielezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Hisham Hendi, wakati akizungumzia matokeo ya jumla ambayo yamehusisha ukuaji wa mapato wa asilimia 0.9 kutokana na utekelezaji thabiti wa mikakati ya kibiashara unaowezeshwa na ukuaji wa idadi ya wateja.

Alisema ukuaji mdogo katika nusu ya pili ya mwaka kwa sehemu kubwa ulitokana na matokeo ya kufungia wateja milioni 2.9 ambao hawajasajiliwa kwa kutumia alama za vidole na gharama zinazohusiana na kukidhi miongozo ya mamlaka pamoja na ushindani mkubwa wa bei.

“Wateja wetu wanaendelea kunufaika na mtandao bora wa kiwango cha juu wa Vodacom kutokana na uwekezaji mkubwa wa Sh. bilioni 154.6 katika kuongeza upatikanaji wa mtandao wa 4G na kuboresha ubora wa mtandao na huduma zetu,” alisema Hendi.

Alisema, kufuatia kuboreshwa kwa huduma za malipo ya kidijitali; Mapato ya M-Pesa yameripotiwa kuongezeka kwa asilimia 7.4 ambayo imechangia asilimia 35.0 katika mapato ya huduma kufikia 2.2pp inayotokana na kuongezeka kwa idadi ya miamala kwa kila mteja.

"Huduma yetu ya M-Pesa imeendelea kutimiza ahadi yake ya kuleta ushirikishwaji wa kifedha nchini, kuwawezesha wateja kufanya miamala kwa urahisi na kuchangia katika kukua kwa uchumi. Kwa sasa tuna wateja milioni 10.1 wanaotumia huduma hii ya M-Pesa ambao wamefanya miamala bilioni 1.4 yenye thamani ya Sh. trilioni 58.1 katika mfumo wa huduma za kifedha kupitia simu za mkononi kwa mwaka," alisema Hendi.

Alifafanua kuwa, Vodacom itaendelea kupanua mfumo wa M-Pesa kwa kutoa huduma zaidi ili kukidhi mahitaji ya sasa ya wateja kwa kadri yanavyoendelea kubadilika.

Alisema kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 ambao unaathiri mataifa na wananchi duniani kote, kipaumbele cha Vodacom ni katika afya na usalama wa wafanyakazi wao wakati wakitoa huduma na msaada kwa wateja wao pamoja na kusaidia serikali pale inapowezekana, kwa ajili ya kukabiliana na hali ya ugonjwa huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live