Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vodacom yamtangaza Hendi kukaimu ukurugenzi mtendaji

16190 Pic+vodacom TanzaniaWeb

Sun, 9 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kampuni ya mawasiliano nchini ya Vodacom imemtangaza Hisham Hendi kuwa kaimu mkurugenzi mtendaji kuanzia  Septemba Mosi.

Tangazo lilitolewa na Vodacom leo katika magazeti linaeleza kuwa Hendi ambaye ana uzoefu wa miaka 15 katika sekta ya mawasiliano, atakaimu nafasi hiyo hadi pale utaratibu wa ajira ya mkurugenzi mtendaji mpya utakapokamilika.

Hatua hiyo imekuja baada ya mkurugenzi mtendaji aliyekuwepo Ian Ferrao kustaafu na aliyetakiwa kuchukua mikoba yake, Sylvia Mulinge ambaye ni raia wa Kenya kukosa vibali vya kufanyia kazi hapa nchini.

Ferrao ambaye aliitumikia kampuni hiyo kwa miaka mitatu baada ya mkataba wake kwisha, alitakiwa kukabidhi mikoba kwa Mulinge kati ya Juni Mosi hadi Agosti 31.

Awali katika taarifa ya kumkaribisha Mulinge, Aprili 9 mwenyekiti wa Bodi ya VodaCom, Ali Mufuruki alisema katika majukumu mapya mteule huyo hana budi kuendeleza mafanikio ya Ferrao ikiwa ni pamoja na kuvutia wawekezaji wengi.

Mulinge alikuwa ni mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa kampuni ya mawasiliano nchini Kenya ya Safaricom aliyojiunga nayo tangu mwaka 2006.

Kuhusu Hendi.

Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Vodacom, Hendi ni mhitimu wa shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Cairo nchini Misri na amekuwa mkuu wa masoko na mauzo wa Vodacom Tanzania tangu mwaka 2016.

Chanzo: mwananchi.co.tz