Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viwanja vya ndege wanolewa mifumo ya serikali

2b701c95785dc0560b0aa835d33a0cb2.png Viwanja vya ndege wanolewa mifumo ya serikali

Sat, 12 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MAMENEJA na Wahasibu 58 wa Viwanja vya ndege vya mikoa wameanza mafunzo ya siku nne ya mifumo mbalimbali ya serikali.

Mafunzo hayo yaliyoanza jana kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TB3) yanalengo la kuwafanya mameneja na wahasibu kuepuka mianya yote ya matumizi mabaya ya fedha na upotevu wa mapato.

Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Biashara wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Shadrack Chilongani alisema washiriki hao wanafundishwa uandaaji wa bajeti (Plan Rep); namna ya kuandaa mpango kazi na mfumo wa ulipaji serikalini (MUSE).

“Haya mafunzo ni muhimu sana kwa washiriki kwani tumekuwa tukitumia mfumo mwingine ambao kwanza ulihusisha maeneo sita pekee yaani JNIA, Makao Makuu, Mwanza, Arusha, Songwe na Mtwara, ambapo kulisababisha kila wakati wa kuandaa bajeti kuwa-

tumia Wahasibu wa JNIA na Makao Makuu kuingiza taarifa za mwaka za mzima za viwanja kwenye mfumo wa EPICOR 10, lakini sasa baada ya mafunzo kila mmoja atafanya peke yake akiwa kiwanjani kwake kila kitu kitakuwa kikionekana Makao Makuu,” amesema

Chilongani Pia amesema mfumo mpya wa ulipaji serikalini utasaidia kuokoa mamilioni ya fedha yaliyokuwa yakipotea kutokana na kuwalipa watu binafsi waliokuwa na mfumo wa awali wa EPICOR 10, uliokuwa ukitumika katika maeneo machache pekee.

Chanzo: www.habarileo.co.tz