Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt Ashatu Kijaji amesema Kutokana na usajili wa viwanda chini ya TIC na EPZA, inategemewa kuwa viwanda vipya vikubwa 500 vitajengwa kufikia mwaka 2025 na kufanya idadi ya sasa ya viwanda vikubwa vinavyoajiri wafanyakazi zaidi ya 500 kuongezeka kutoka 41 hadi kufikia 541.
Dkt Kijaji amesema Tayari Serikali ya Awamu ya Sita imekwishaanza utekelezaji wa Kongani kubwa ya Viwanda ya Kwala ambayo itakuwa na viwanda 200 vikubwa kwa ajili ya kutengeneza nguo, vifaa vya umeme, vifaa vya ujenzi, dawa na aina nyingine.
Aidha Dkt Kijaji amesema Mradi huo umekwishaanza na awamu ya kwanza itakamilika ifikapo mwaka 2024 na viwanda vitatoa ajira za moja kwa moja 100,000 na zisizo za moja kwa moja 300,000.
Uwekezaji katika eneo hilo unakadiriwa kugharimu Dola za Marekani Bilioni 3 na unalenga kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha bidhaa za viwanda katika Soko la Pamoja la Afrika. - Amesema Dkt Kijaji.
Waziri Dkt Ashatu Kijaji ameyasema hayo leo Bungeni Dodoma wakati akiwasilisha Makadirio, Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo ya mwaka 2022/2023