Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viwanda vidogo kumaliza uhaba wa sukari nchini

Light Brown Sugar.jpeg Viwanda vidogo kumaliza uhaba wa sukari nchini

Sat, 28 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mwishoni mwa mwaka huu wa fedha, mtambo wa awali wa kuzalisha sukari utakaoendeshwa na wakulima wadogo utakamilika ikiwa ni moja ya hatua kuanzisha viwanda vidogo vya sukari nchini.

Hatua hiyo inalenga kumaliza uhaba wa sukari uliopo kwa matumizi ya ndani ya zaidi ya tani 300,000.

Wizara ya Viwanda na Biashara inasema lengo ni kufikia tani zaidi ya 700,000 ifikapo mwaka 2025.

Hivi karibuni Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhandisi na Ubunifu Mitambo Tanzania (Temdo), Profesa Frederick Kahimba, alinukuliwa akisema hatua hiyo ni utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo chini ya Dira ya Taifa ya Mwaka 2025.

Mpango huo unalenga kujenga uchumi shindani wa kutegemea viwanda kwa maendeleo ya taifa.

Alisema mitambo hiyo midogo imewalenga wakulima wadogo katika maeneo yanayozalisha miwa kwa wingi ikiwamo mikoa ya Morogoro, Kilimanjaro na Kagera.

Mtambo mmoja utauzwa kwa Sh milioni 250. Mtambo kama huo ukiagizwa nje ya nchi, hugharimu Sh milioni 400 hadi milioni 500.

Mtambo wa awali utakamilika mwishoni mwa mwaka huu wa fedha. Hadi sasa uundwaji wa mtambo huo wa awali umefikia asilimia 40.

Chanzo: www.habarileo.co.tz