Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viwanda na biashara wakutana na wadau sekta ya nguo

B5b85b48da89aca4cb81b76ff1b90dd0 Viwanda na biashara wakutana na wadau sekta ya nguo

Thu, 11 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amekutana na kufanya mazungumzo na wadau wa sekta ya nguo na mavazi kwa lengo la kuboresha na kukuza sekta hiyo.

Pia amewataka wafanyabiashara wanaoagiza nguo na mavazi kutoka nje hususani vitenge kufanya biashara kwa karibu na wenye viwanda vinavyozalisha bidhaa hizo hapa nchini.

Akizungumza na wadau hao katika kikao kilichofanyika juzi jijini hapa, Kigahe alisema hatua hiyo ni katika kuboresha na kukuza sekta ya nguo na mavazi ili kukidhi mahitaji ya nchi.

"Kama mnavyofahamu kwa sasa mahitaji ya nguo na mavazi ni mengi sana hapa nchini kuliko uzalishaji tulionao na ndio sababu nikaona nikutane nanyi.Hivyo kupitia kikao hiki ni fursa ya mimi kuwasikiliza, hivyo nawataka ninyi muwe huru kuwasilisha changamoto walizonazo ili serikali iweze kuzishughulikia na hivyo kuzalisha kwa tija,"alisema.

Aidha, Kigahe aliitaka Jumuiya ya Wafanyabiashara na Chama cha Wazalishaji wa Nguo (Tegamat) kuwasilisha wizarani mipango mikakati ya kuboresha na kuendeleza viwanda na biashara katika sekta hiyo ili kukuza uchumi wa nchi.

Kigahe alitumia fursa hiyo kutoa rai kwa wafanyabiashara wanaoagiza nguo na mavazi kutoka nje hususani vitenge kufanya biashara kwa karibu na wenye viwanda vinavyozalisha bidhaa hizo hapa nchini ili kuboresha ubora wa nguo kulingana na mahitaji ya soko.

"Pia niwasihi wenye viwanda vinavyozalisha nguo na mavazi kuongeza uzalishaji wa nguo bora na zenye viwango na kutosheleza mahitaji ya soko la ndani na kuuza nje ya nchi, kwani sekta hii ndio sekta inayotoa ajira nyingi za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa wananchi,”alisema.

Katika kikao hicho kilichojumuisha wadau ambao ni watengenezaji na waagizaji wa nguo na mavazi kutoka ndani na nje ya nchi, wadau hao waliwasilisha changamoto na mapendekezo yao kwa Naibu Waziri wakiwa na lengo la kuboresha na kukuza sekta hiyo.

Aidha, alisema serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali katika kuendeleza sekta ya nguo na mavazi nchini ikiwemo kukuza soko la ndani la bidhaa hizo pamoja na kuandaa na kutekeleza Mkakati wa kuendeleza Sekta ya pamba nguo hadi mavazi na kuuhuisha ambapo utekelezaji wake utaanza mwaka 2021 - 2032.

Chanzo: habarileo.co.tz