Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viwanda 20 vyaingizwa sokoni kusaka wawekezaji

Viwanda Serikali yanadi viwanda 20

Tue, 24 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Serikali imewaita wawekezaji kutoka sekta binafsi wawekeze katika viwanda 20 vilivyobinafsishwa na sasa vimerudishwa serikalini.

Viwanda hivyo ni kati ya viwanda 156 vilivyobinafsishwa kwa mujibu wa sera iliyotekelezwa miaka ya 1990 nchini. Viwanda 68 havikujiendesha kwa mujibu wa mikataba na 88 vilifanya vizuri.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo jana alisema kati ya viwanda hivyo 68

ambavyo havikufanya kazi vizuri, 48 wawekezaji hawakuzingatia matakwa ya mikataba na 20 kati ya hivyo tayari vimerejeshwa serikalini.

“Baadhi ya viwanda vilikosa sifa ya kuwa viwanda baada ya kubinafsishwa miaka ya 1990. Timu ya serikali iliundwa na ikaingia katika mazungumzo na wawekezaji na kukubaliana kurudisha kisheria viwanda hivyo serikalini. Tayari viwanda 20 vimerejeshwa serikalini havina migogoro vipo mikononi mwa serikali,” alisema Profesa Mkumbo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz