Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vivuko kutatua changamoto usafiri Kanda ya Ziwa

Misungwiiiiiiii Vivuko kutatua changamoto usafiri Kanda ya Ziwa

Tue, 28 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kukamilika kwa ujenzi wa vivuko vipya vinne na ukarabati wa vivuko vinne vitakavyotoa huduma katika maeneo mbalimbali ya Ziwa Victoria kutapunguza changamoto za usafiri kwa wananchi wanaoishi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na kutarahisisha shughuli za maisha kwa urahisi, uhakika na usalama.

Hayo yamesemwa mkoani Mwanza na Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya, wakati alipokagua karakana ya ujenzi wa meli na vivuko ya Songoro na kupata taarifa ya maendeleo ya ujenzi na ukarabati wa vivuko hivyo vitavyogharimu takribani bilioni 26 na kutarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Agosti mwaka huu.

“Nimekagua na nimeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa vivuko vipya lakini pia na ukarabati wa vivuko unaoendelea, nimatumaini yangu vivuko hivi vitakamilika ndani ya muda kwani kuna baadhi ya maeneo vivuko hivyo havipo au kimebakia kimoja na hivyo kutokidhi mahitaji ya wananchi", amesema Kasekenya.

Amefafanua kuwa kwa sasa ujenzi wa vivuko hivyo unaendelea na vipo katika hatua mbalimbali na kutaja kuwa vivuko hivyo ni Kisorya – Rugezi (Ukerewe - Mwanza), Ijinga – Kahangala (Magu - Mwanza), Bwiro – Bukondo (Ukerewe - Mwanza) na Nyakalilo – Kome (Buchosa - Mwanza).

Aidha, ukarabati wa vivuko unaoendelea ni pamoja na MV Misungwi (Kigongo - Busisi), MV Mara (Iramba - Majita), MV Ujenzi (Kisorya - Rugezi) na MV Nyerere (Bugolora - Ukara).

Aidha, ameiagiza Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), kumsimamia mkandarasi wa Kampuni ya Songoro kufunga vifaa vyote vilivyosanifiwa kuanzia katika hatua za awali hadi vivuko hivyo vitapokamilika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live