Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita Urusi na Ukraine kuongeza mahitaji ya dhahabu

Madini Pic Data Vita kuongeza mahitaji ya dhahabu

Fri, 29 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Madini, Dotto Biteko leo Bungeni Dodoma amesema changamoto ya vita kati ya Urusi na Ukraine inaweza kusababisha mahitaji makubwa ya madini ya dhahabu.

"Uchumi wa madini nchini kwa kiasi kikubwa unatokana na madini ya dhahabu, ambayo huchangia takribani asilimia 80 ya mapato yatokanayo na rasilimali madini, Wachambuzi wa masuala ya uchumi duniani walitarajia bei ya dhahabu kuendelea kuwa tulivu kwa mwaka 2022, hata hivyo, bei ya madini ya dhahabu imepanda kutoka wastani wa dola za Marekani 1,412.98 Julai 2019 hadi kufikia 1,947.83 Machi, 2022

"Kuongezeka kwa bei ya dhahabu kunatokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwepo wa UVIKO-19, vita kati ya Urusi na Ukraine inaweza kusababisha mahitaji makubwa ya madini ya dhahabu, hii ni kwa sababu watu na taasisi duniani hupendelea kuhifadhi thamani ya fedha zao katika madini ya dhahabu kwa kuwa ni amana iliyo salama zaidi hasa wakati wa mitikisiko ya kiuchumi"

"Kwa upande mwingine, ukuaji wa teknolojia umesababisha ongezeko la mahitaji ya madini ya palladium, nickel, aluminium, cobalt na madini ya kinywe (graphite), hivyo, bei ya madini hayo inatarajiwa kupanda na kuongeza fursa za uwekezaji" Waziri Biteko

Chanzo: www.tanzaniaweb.live