Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Visiwa 16 vyakodishwa zanzibar

Kisiwa Kukodishwaaaaa Visiwa 16 vyakodishwa zanzibar

Mon, 27 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumla ya visiwa vidogo 16 vimekodishwa kwa wawekezaji katika miradi ya ujenzi wa hoteli za kitalii Zanzibar katika kipindi cha miaka miwili sasa, huku wamiliki wake wakitakiwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira ili kuepukana na athari zinazoweza kujitokeza ikiwemo za mabadiliko ya tabia ya nchi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Mudrik Ramadhan Soraga amesema wakati alipozungumza na mwekezaji wa kisiwa cha Changuu pamoja na Bawe baada ya kukabidhiwa kisiwa hicho kwa shughuli za uwekezaji.

Soraga alisema Zanzibar inakabiliwa na tishio la athari za mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo suala la uhifadhi wa mazingira ikiwemo fukwe na mazao ya baharini kwa ujumla wake unahitajika. Alisema baadhi ya visiwa kabla ya kukodishwa kwa wawekezaji, wavuvi walikuwa wakiendesha uvuvi haramu pamoja na uharibifu mkubwa wa matumbawe na hivyo kusababisha uhaba wa samaki.

“Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inasisitiza na kuwataka wawekezaji wote kabla ya kutekeleza miradi ya uwekezaji kuhakikisha kwamba wanawasilisha mpango kazi wa mazingira ambao ndio mwongozo wa kazi,” alisema

Chanzo: www.tanzaniaweb.live