Wizara ya Kilimo kupitia Bajeti yake ya mwaka 2023/2024 imenunua vishikwambi 4446, kati ya hivyo 946 vimeshasambazwa na usambazaji unaendelea kwa ajili ya kutumika kwa shughuli mbalimbali ikiwemo usajili wa wakulima.
Taarifa zinaonesha kwamba vishikwambi hivyo vitatumika pia kukusanyia taarifa, kuchukua alama ya nukta katika mashamba ya wakulima na utoaji huduma za ugani kwa njia ya kidijiti, hatua itakayowawezesha maofisa ugani katika ngazi ya kata kukusanya na kuingiza takwimu kwenye mfumo wa ARDS (Agricultural Routine Data System).
Aidha, katika kuhakikisha wakulima wanafanya kilimo chenye tija, taarifa zinaonesha kwamba Wizara ya Kilimo imeanzisha kituo cha huduma za ushauri kwa wakulima (call centers) na kununua vifaa vya huduma za ugani katika halmashauri 166 nchini.