Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wakuu waanza kuwasili ukumbini kushiriki mkutano Sadc

71824 Viongozi+pic

Sat, 17 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Viongozi wakuu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) wameanza kuwasili katika ukumbi wa Julius Nyerere kushiriki mkutano wa 39 wa jumuiya hiyo na kupokewa na mwenyeji wao Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Viongozi waliowasili katika mkutano huo unaofanyika kwa siku mbili, leo Jumamosi Agosti 17, 2019 na kesho ni Rais wa Comoro, Azali Assoumani; Rais wa Zimbabwe, Emmason Mnangagwa na Edgar Lungu wa Zambia.

Viongozi wa Serikali ya Tanzania waliopo ukumbini ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.

Pia, wapo marais wastaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na rais mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Aman Karume.

Katika mkutano huo pia wapo mawaziri wakuu wastaafu, Joseph Warioba na Cleopa Msuya pamoja na wakuu wa majeshi wastaafu, Davis Mwamunyange na George Waitara na katibu mkuu mstaafu, Ombeni Sefue.

 

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz