Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa Afrika waweka mkakati wa kuimarisha uzalishaji wa mbolea

Fdfg.jpeg Viongozi wa Afrika waweka mkakati wa kuimarisha uzalishaji wa mbolea

Sat, 11 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Marais wa nchi tano za Afrika na wakuu wa serikali wamehudhuria mkutano wa Kilele wa kujadili ubora wa udongo na mbolea barani Afrika, wakitoa wito wa uwepo wa mkakati wa pamoja, hatua za pamoja na uwekezaji ili kuiwezesha Afrika kuzalisha chakula cha kutosha.

Mkutano huo unaofanyka mjini Nairobi Kenya unahudhriwa na marais wa nchi tano za Afrika akiwemo Hakainde Hichilema wa Zambia, Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe, Nangolo Mbumba wa Namibia, Dkt Lazarus Chakwera wa Malawi na Faustin-Archange Touadéra wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, pamoja na mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat.

Katika mktano huo rais Hichilema wa Zambia amesema inastaajabisha kuwa mataifa mengi ya Afrika bado yanaendelea kuagiza kwa wingi mbolea kutoka mataifa ya nje licha ya uwezo wake wa kujitegemea kuzalisha chakula cha kutosha, na kutoa wito kwa mataifa ya Afrika kufanya biashara kwa pamoja ikiwa ni sehemu ya kuinua uwezo wa nchi husika katika uzalishaji wa chakula barani Afrika.

Rais wa Kenya William Ruto amesema katika mkutano huo kwamba, Afrika inapaswa kujitahidi kupata mbolea ya bei nafuu, bora na inayoweza kupatikana kwa urahisi kwa utengenezaji wa ndani ya mataifa ya Afrika, hatua ambayo itaongeza tija na uzalishaj na kufanya Afrika ijitosheleze kwa chakula.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live