Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Vilainishi visivyo na ubora chanzo uharibifu wa injini’

7f06a2ba1be361359b7d6246d68f486c ‘Vilainishi visivyo na ubora chanzo uharibifu wa injini’

Tue, 7 Jun 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Matumizi ya vilainishi vya magari visivyo na ubora, imeelezwa kuwa ni chanzo cha kuharibika kwa injini nyingi za magari.

Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam leo na Meneja bidhaa wa Kampuni ya Toyota Tanzania, Nadah Ndiyebi, wakati wa hafla ya kuingia mkataba wa miaka mitatu kati ya kampuni hiyo na Kampuni ya mafuta ya AFROIL kwa ajili ya kusambaza na kuuza mafuta ya injini yaitwayo Toyota Genuine Motor Oil (TGMO), kwa nchi nzima.

Meneja huyo amesema dhumuni la ushirikiano huo ni kupanua wigo wa bidhaa zao na kuwarahisishia wateja wao upatikanaji wa vilainishi hivyo kwa urahisi.

“Toyota Genuine Motor Oil (TGMO), ndio mafuta ya injini yaliyotengenezwa kisayansi na kujaribiwa kwa uthabiti, ili kuhakikisha ulinganifu bora zaidi kwa mahitaji,”amesema Ndiyebi.

Kwa upande wake Meneja Vilainishi wa Kampuni ya Toyota Tanzania, Anam Mwemutsi ameeleza walikuwa wanashindwa kuwafikia wateja wao nchi nzima kwa sababu ya matawi machache waliyokuwa nayo, hivyo kuungana na AFROIl, kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuwafikia wateja wao nchi nzima.

Mwemutsi ameeleza kuwa vilaishi hivyo vinasaidia kuweka ulinzi, vina nguvu na husaidia kupunguiza kiwango cha nishati inayopotea, na kupunguza matumizi makubwa ya matengenezo.

Amesema baadhi ya vilainishi visivyo na ubora, husababisha injini kupata moto, lakini vilainishi vya TGMO, injini ya gari husika haiwezi kuchemka kiasi hicho, lakini pia itaepusha msuguano wa vyuma ndani ya injini.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa AFROIL, Lufti Binkleb amesema kuwa makubaliano hayo na Toyota yatazinufaisha kampuni zote mbili katika kutoa huduma kwa wateja wao na kwamba TGMO sasa inatapatikana katika vituo vyote vya mafuta vya AFROIL nchi nzima.

Chanzo: www.habarileo.co.tz