Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vikwazo visivyo vya kifrodha kumalizwa EAC

Uchumi Kupanda Vikwazo visivyo vya kifrodha kumalizwa EAC

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka mawaziri na watendaji wanahusiana na masuala ya biashara na forodha kuhakikisha wanakutana na kumaliza vikwazo vyote ambavyo sio vya kiforodha baina ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Aliyasema hayo wakati wa Mkutano wa 23 wa kilele wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais Samia amesema, wananchi wa Afrika Mashariki wanataka kufanya biashara kwenye mazingira rafiki na sio vikwazo.

Rais Samia amesema, Nchi za Afrika Mashariki zina mambo mengi ya kufanana kuliko ya kutofautiana hivyo ni wakati sasa vikwazo hivyo viondolewe ili kuruhusu bishara baina ya nchi wanachama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live