Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijiji 140 Manyara vyanufaika na mradi wa Rea

11462 Umeme+pic TanzaniaWeb

Mon, 16 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Babati. Vijiji zaidi ya 140 wilayani Babati Mkoa wa Manyara vimenufaika na mradi wa wakala wa umeme vijijini (Rea) na ujenzi wa zahanati mpya 18 na vituo vya afya tisa.

Hayo yameelezwa jana Jumamosi Julai 14, 2018 na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2017/18 katika kikao cha halmashauri kuu ya mkoa huo.

Amesema mkoa huo pia umefanikisha mpango wa kuwapatia matibabu bure wazee wasiojiweza na wenye umri wa zaidi ya miaka 60 wanaoishi Wilaya za Babati, Mbulu, Kiteto, Hanang' na Simanjiro.

“Ilani imetekelezwa kwa kiasi kikubwa hata kwenye suala la maji, elimu na kilimo na mifugo tumepiga hatua pamoja na kutatua changamoto za wananchi wetu kwa kuwasikiliza na kutekeleza kilio chao," amesema Mnyeti.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz