Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Vijana ni nguzo muhimu maendeleo ya uchumi’

Mwinyi Pc Data.png ‘Vijana ni nguzo muhimu maendeleo ya uchumi’

Fri, 6 Jan 2023 Chanzo: Habarileo

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi, ameahidi kushirikiana na vijana katika kufanya kazi za ujenzi wa maendeleo ya taifa kwa lengo la kuwainua kiuchumi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa matembezi ya vijana leo Januari 5, 2023 Zanzibar, Dk Mwinyi amesema vijana ni nguzo muhimu katika kusukuma maendeleo ya uchumi.

Matembezi hayo yaliyozinduliwa ni miongoni mwa shamrashamra za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo kilele chake ni Januari 12 mwaka huu.

Pia Rais Mwinyi aliwasihi vijana kujiweka imara na kujitambua huku akisema wana nafasi kubwa ya kulitumikia taifa na kuliletea maendeleo.

“Shikamaneni na saidianeni, jitengezeeni ajira ili muweze kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili,” Dk Mwinyi alisema.

Pia alisema serikali imedhamiria kuwainua vijana kwa kuwapatia fursa za ajira kwa namna iliyo bora na sahihi kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

“Serikali itawapatia mikopo itakayowaendeleza na tutazisimamia mamlaka husika, ili ziwape kipaumbele kwenye wepesi wa kupata hiyo,” aliongeza.

Chanzo: Habarileo