Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijana kaya zisizojiweza kupatiwa ufumbuzi kiuchumi

Fedhapic Vijana kaya zisizojiweza kupatiwa ufumbuzi kiuchumi

Sun, 6 Aug 2023 Chanzo: Mwananchi

Vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19 wanaosoma na wasiosoma sasa kupatiwa ufumbuzi utakaowainua kiuchumi ili kujiepusha na tabia zisizofaa zikiwemo matumizi ya dawa za kulevya na wizi. Vijana hao ambao wanatoka kaya masikini wanalengwa kusaidiwa kupatiwa mianya ya kiuchumi ikiwemo ujasiriamali na mitaji kupitia mradi wa Ahadi wa Shirika la misaada ya kibinadamu la World Vision. Mbali na hayo, kundi hilo ambalo ni vijana waliobalehe linaangaziwa kupatiwa elimu ya afya ya uzazi kujikinga na magonjwa ya zinaa na mimba za utotoni.

Vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 19 wanaosoma na wasiosoma sasa kupatiwa ufumbuzi utakaowainua kiuchumi ili kujiepusha na tabia zisizofaa zikiwemo matumizi ya dawa za kulevya na wizi. Vijana hao ambao wanatoka kaya masikini wanalengwa kusaidiwa kupatiwa mianya ya kiuchumi ikiwemo ujasiriamali na mitaji kupitia mradi wa Ahadi wa Shirika la misaada ya kibinadamu la World Vision. Mbali na hayo, kundi hilo ambalo ni vijana waliobalehe linaangaziwa kupatiwa elimu ya afya ya uzazi kujikinga na magonjwa ya zinaa na mimba za utotoni. Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa World Vision nchini, James Anditi alisema watawapatia nafasi ya kupata ajira ikiwemo kilimo ufugaji na kazi za mikono. “Hii ni nafasi kubwa kwa vijana na nawaomba waje waone fursa zilizopo, tunajua wanavipaji mbalimbali tunawawezesha wapate mikopo. “Tunawezesha vijana wawe na fikra adilifu kwasababu mara nyingi wanajiona kama watu ambao hawajiwezi na wamesahaulika. Tunaleta matumaini kwao, kwasababu tunajua wana talanta mbalimbali,” alibainisha Anditi alipokutana na wadau mbalimbali. Kwa upande wa Serikali, Peter Ugata ambaye ni Mratibu wa Huduma za Ajira Kitengo cha Huduma za Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu (TAESA), alisema Serikali inatoa mafunzo kwa vijana kwaajili yakupata uzoefu wa kazi kwa muda wa mwaka mmoja. Alisema vilevile kwa wale vijana walio na ujuzi wa chini na wasio na ujuzi, Serikali inawaunganisha na fursa za ajira ambao hadi sasa zaidi ya vijana elfu kumi wameshanufaika. Ugata alisema kupitia mradi wa Ahadi vilevile utawajengea uwezo wa kuajirika na kujiajiri ambapo itawasaidia katika kushindana kwenye soko la ndani. “Wito wetu kama Serikali kupitia kitengo cha ajira tunawaomba waajiri waweze kuwatumia hawa vijana kwa lengo la kuwapatia ujuzi wa kazi ambayo tunaweza kuwa na nguvu kazi kubwa tutakayoitumia kwa maendeleo ya nchi yetu” alisema. Naye, Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto Kanda ya Mashariki, Joyce Mwehanga alisema kwa upande wa afya ya uzazi mtindo wa maisha ya sasa umegubikwa na utamdawazi ambapo watoto ni rahisi kuona yanayoendelea mitandaoni ambayo mengine hayana maadili ya nchi. Mwehanga alisema lengo kubwa ni kupewa uelewa juu ya afya ya uzazi ambayo itawasaidia kuepukana na mimba za mapema pamoja na maradhi. “Maisha yetu kwa sehemu kubwa watoto hawapati elimu hio kutoka kwa wazazi wao. Mradi huu unaleta tija kwa vijana wetu kujielewa na kuelewa afya ya uzazi kwa njia sahihi.” alisema.

Chanzo: Mwananchi