Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Video: Serikali yapiga ‘STOP’ utoaji wa passport

Thu, 25 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesimamisha utoaji hati za kusafiria “Passport” za jumla na makundi kwa muda, huku akidai kuwa vijana wanapoenda nje ya nchi, wanafanyishwa kazi zisizo za maadili.



Waziri Mwigulu ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari, Makao Makuu ya Ofisi za Uhamiaji yaliyopo Kurasini Jijini Dar es salaam.

Aidha Waziri Nchemba alisema kuwa hawaruhusu kuona raia wanakwenda katika nchi mbalimbali alafu wanapata manyanyaso.

“Hatufurahishwi kuona raia wetu wanakwenda katika nchi mbalimbali kwa utaratibu uliozingatia sheria halafu wanapata manyanyaso. Nataka wanaofanya ukatili huu wa kuwarubuni watu wetu watafutwe na wachukuliwe hatua,“ amesema Waziri Mwigulu Nchemba.

Chanzo: bongo5.com