Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Puma Tanzania kusaka zaidi soko SADC

Tue, 6 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kampuni ya Puma Energy Tanzania inayozalisha bidhaa za mafuta na vilainishi  katika nchi 13 za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) imesema imeanza kujitangaza ubora wa bidhaa zake kupitia maonyesho ya bidhaa katika  wiki ya viwanda kwa jumuiya hiyo.

Kampuni hiyo yenye ubia na Serikali ya Tanzania ilianza kufanya biashara zake nchini mwaka 2011 baada ya kununua hisa zote za iliyokuwa Kampuni ya BP katika nchi za SADC isipokuwa Msumbiji na Afrika Kusini. Inauza mafuta ya taa, Dizeli, vilaini vya magari huku ikimiliki vituo 52 vya mafuta Tanzania.

Meneja wa Mahusiano ya Kampuni pamoja na huduma za Kisheria, Godluck Shirima akizungumza jana Jumatatu Agosti 5, 2019 katika siku ya kwanza ya maonyesho ya biashara ya viwanda kwa nchi 16 za SADC, Dar es Salaam nchini Tanzania alisema kampuni hiyo imeendelea kuwa imara katika ushindani wa soko la SADC baada ya kukuza mtandao na bidhaa zake.

“Ukuaji huo umeonekana kupitia ongezeko la gawio kwa wanahisa wake, mwaka 2011/12 Puma ilitoa gawio la Sh3.5 bilioni huku Serikali ikichukua asilimia 50, lakini mwaka 2018/19 Puma imetoa gawio la Sh22 bilioni huku Serikali ikichukua asilimia 50,”alisema.

“Tunachokifanya katika maonyesho haya ni kuhakikisha tunakuza mtandao wa bidhaa zetu na tunahitaji kueleza ubora wa bidhaa zetu zaidi , kwa sababu tunatambulika katika Shirika la viwango Duniani(ISO).”

Tayari washiriki 3001 kutoka nchi hizo ikiwamo Tanzania wamekeza, na kati yao, wafanyabiashara 1,500 wameanza kuonyesha bidhaa zao katika viwanja vya Karimjee, GymKana na Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere(NJICC).

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz