Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: ATCL ilivyopata dili kusafirisha wanajeshi

Fri, 17 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Ladislaus Matindi ameeleza kuwa haikuwa kazi rahisi kwa shirika hilo kupata zabuni ya kusafirisha askari 217 wa Jeshi la Wananchi Tanzania (Jwtz) kwenda Darfur, Sudan kulinda amani.

Matindi alisema hayo jana wakati wa kuaga kundi la kwanza la askari hao na maofisa wanaoelekea Darfur, shughuli iliyofanyika iliyofanyika katika uwanja wa ndege wa jeshi wa Airwing, Ukonga, jijini Dar es Salaam.

Alisema kuna mashirika makubwa ya ndege yangeweza kufanya kazi hiyo, lakini Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo na watendaji wake walifanya kazi kubwa kuushawishi Umoja wa Mataifa (UN), kwamba Tanzania ina ndege nzuri itakayoweza kuwabeba askari na kuwapeleka Sudan.

“Jenerali Mabeyo, mnadhimu mkuu wa jeshi, mkuu wa operesheni na mafunzo na watendaji wengine wameipigania ATCL kuhakikisha inashiriki kikamilifu mchakato huu. Haikuwa rahisi kama vile chakula kwenye sahani, kuna kazi kidogo ilifanyika kwa uaminifu na uzalendo.”Mkuu wa Operesheni na Mafunzo JWTZ, Meja Jenerali Alfred Kapinga alisema ni mara ya kwanza kwa askari hao kusafiri na ATCL tangu kuanza kwa operesheni za UN za kulinda amani miaka 12 iliyopita.

Chanzo: mwananchi.co.tz