Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uzalishaji wa sukari waongezeka nchini

Sukarii Sukari Leseni Uzalishaji wa sukari waongezeka nchini

Sun, 16 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan kutaka nchi ijitosheleza kwa uzalishaji wa sukari yameanza kutekelezeka baada takwimu kuonesha kuwa kiwanda cha sukari cha Kagera Sugar kimeongeza uzalishaji kutoka tani 60,000 hadi tani 110,000.

Majaliwa ametoa maelezo hayo jana Jumamosi, Oktoba 15, 2022) alipofanya ziara ya kukagua upanuzi wa mashamba ya miwa na mitambo na iliyoongezwa kwa ajili ya uzalishaji wa sukari katika kiwanda cha Kagera Sugar kilichopo Misenyi, mkoani Kagera.

Amesema kitendo cha kampuni hiyo kuendelea kuweka mikakati ya kuboresha na kukuza uwekezaji ni kizuri kwani kwa kiasi kikubwa kitawezesha kuongeza kiwango cha uzalishaji wa sukari nchini na kuipungua Serikali gharama ya kuagiza kutoka nje.

Waziri Mkuu amesema kuwa uwepo wa kiwanda hicho ni fursa ya kiuchumi kwa wakazi waishio katika vijiji jirani na kiwanda hicho ambao wanajiajiri kupitia kilimo cha miwa kwa kuwa wana uhakika wa soko kiwandani hapo.

“Endeleeni kuiunga mkono Serikali kwa kuongeza fursa za ajira kupitia kiwanda chenu.”

“Uwekezaji wenu utawezesha kuongeza kiwango cha uzalishaji wa sukari nchini, hii itawezesha nchi kupunguza kiwango cha sukari tunachoagiza kutoka nje. Mkakati wenu wa upanuzi wa kiwanda uende sambamba na ushirikishwaji wa wananchi waishio katika vijiji vinavyowazunguka ili nao waongeze mashamba ya miwa,” amesema Waziri Mkuu.

Hata hivyo, Majaliwa amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Kanali Wilson Sakulo kuweka mkakati wa kuhamasisha wananchi wa vijiji 13 vinavyozunguka kiwanda hicho kulima zao la miwa kwa wingi ili kujiongezea kipato na uwepo wa malighafi ya inayohitajika kiwandani hapo.

Amewahakikishia viongozi wa Chama cha Mapinduzi kuwa Serikali itaendelea kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa lengo la kuhakikisha yale yote yaliyo ahidiwa yanatekelezwa.

“Viongozi wangu wa CCM sisi tutaendelea kumsaidia Rais Samia kuhakikisha yote yaliyoahidiwa yanatekelezwa.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live