Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uzalishaji wa mpunga waongezeka maradufu

MPUNGA Uzalishaji wa mpunga waongezeka maradufu

Fri, 24 Mar 2023 Chanzo: mwanachidigital

Wakulima wa mpunga katika Kijiji cha Dihombo na Kigugu, Wilaya ya Mvomero wameeleza namna uzalishaji ulivyoongezeka kutoka gunia nane hadi gunia 25 kwa hekari ambapo wamesema kuwa kuwepo mradi wa 'Farm to market Alliance' unaotekeleza na Shirika la Farm Africa umesaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza uzalishaji huo.

Akizungumza katibu wa kikundi cha cha wakulima wa mpunga skimu ya Kigugu Khadija Hamis amesema kuwa kupitia mradi huo wa 'Farm to market Alliance' wakulima wameweza kuunganishwa na watoa huduma za kilimo ikiwepo Taasisi ya Utafiti wa Kilimo cha Mpunga (Tari Dakawa) na makampuni mengine ya zana za kisasa za kilimo na pembejeo.

Hadija amesema kuwa kupitia wadau hao wameweza kupata mafunzo ya matumizi ya teknolojia bora za kilimo ikiwemo matumizi ya mbegu bora za mpunga, pembejeo, viatilifu na pia namna ya kutapa masoko.

Amesema Katika skimu hiyo ya Kigugu chanzo kikubwa cha maji ni mto chazi na kwamba shughuli za kilimo hufanyika mara mbili kwa mwaka, hata hiyo kutokana na mabadiliko ya tabia nchi kiasi cha maji katika mto huo kimepungua na hivyo kufanya eneo la kilimo kuwa ni hekta 661 wakati skimu hiyo inaukubwa wa hekta 800.

Amesema kupitia Tari wakulima wameweza kupatiwa mbegu bora 5 za mpunga ambazo kwa sasa zipo kwenye majaribio kupitia shamba darasa na zote zinaonekana kukua vizuri na kustahamili magonjwa.

Naye mkulima kutoka Kijiji cha Dihombo, Ramadhan Opole ameiomba Serikali kusimamia bei ya mpunga hasa wakati wa mavuno ili kudhibiti wafanyabiashara wanaokwenda mashambani kununua mpunga kwa kupanga bei.

"Uzalishaji wa mpunga unagharama kubwa kuanzia kuandaa shamba mpaka kuvuna mkulima anaweza kutumia hata milioni mbili lakini cha kusikitisha mfanyabiashara anapokuja kununua tayari anakuja na bei yake tena ya kumkandamiza mkulima hivyo mkulima anajikuta analima kwa hasara," amesema Opole.

Awali akitoa taarifa ya mradi huo mkurugenzi wa Shirika la Farm Africa Mary Barton amesema kuwa mradi huo unawashirika sita watu wa Mpango wa Chakula duniani (WFP).

Mary ameeleza malengo ya mradi huo kuwa ni kuwajengea uwezo wakulima wa matumizi ya teknolojia bora za kilimo ili kuondokana na kilimo cha mazoea ambacho hakina tija kiuchumi.

Akizungumza kwa niaba ya Serikali ya mkoa wa Morogoro kaimu tawala anayeshughulikia kilimo na uzalishaji Dk. Rozalia Rwegasila amesema kuwa mkoa wa Morogoro ndio mkoa unaoongoza kwa uzalishaji wa mpunga ambao umekuwa ukitumika kwa matumizi ya ndani na nje ya nchi.

Hata hivyo Dk. Rozalia amesema kuwa asilimia 80 ya wakulima wa Mkoa wa Morogoro wanategemea mvua hivyo Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha miundombinu ya umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji.

Chanzo: mwanachidigital