Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uzalishaji mpunga ndani waongezeka maradufu

Wakulima Wa Mpunga Wapata Hasara Ya Mamilioni 1536x1028 Uzalishaji mpunga ndani waongezeka maradufu

Mon, 6 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MTEKNOLOJIA wa mbegu kutoka Wakala wa Mbegu za Kilimo wa Serikali (ASA), Grace Matima, amesema uzalishaji wa ndani kwa zao la mpunga umeongezeka kutoka tani 581 hadi 1,436.

Hayo aliyaeleza mwishoni mwa wiki alipokuwa akizungumza na wakulima wa zao hilo katika mabonde ya mpunga ya Kibondemzungu na Mtwango, visiwani Zanzibar.

Alisema hatua hiyo imefanikiwa kutokana na wakulima kulima kwa wingi zao hilo.

Alisema tangu kuanzishwa kwa ASA kumeongeza uzalishaji kutoka asilimia 3-9 na kusema kuwa ni faraja kubwa kufikia malengo.

Alisema serikali zote mbili zimekuwa zikishirikiana kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora na zenye tija ili kuwainua wakulima wa zao hilo kimaisha na familia zao.

"Uzalishaji wa mbegu bora umeongezeka, na uagizaji wa mpunga kutoka nje umepungua kwa asilimia 19, hivyo ni faraja kwetu kuona tumetimiza lengo letu," alisema Matima.

Vilevile, alisema Zanzibar kuna ongezeko kubwa la utumiaji wa mbegu kutoka tani 75 mpaka 248 kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2017-2019.

Meneja wa shamba la mbegu Kilangali Kilosa, Aneth Molela, alisema wameridhishwa na utumiaji wa mbegu Zanzibar na kuwapa matumaini ya kuongeza uzalishaji kutokana na kujengwa kwa miundombinu mipya.

Alisema, wataendelea na uzalishaji wa miundombinu kwa msaada wa Benki ya Dunia na kuamini kwamba utaongeza tija kwa kutoagiza chakula kutoka nje.

Alisema upokeaji wa mbegu unasaidia kutoa mchango wa uzalishaji ndani na kupunguza kutoka nje.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live