Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uzalishaji mazao ya chakula wapungua kwa tani milioni 15

Ghala La Chakula Uzalishaji mazao ya chakula wapungua kwa tani milioni 15

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Dk Ashatu Kijaji amesema ongezeko la bei ya bidhaa za vyakula kwa mwaka 2021/22 ulichangiwa na upungufu wa uzalishaji wa bidhaa hizo kwa wastani wa tani milioni 1.52 ukilinganisha na tani milioni 18.67 zilizozalishwa mwaka 2020/21.

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Dk Ashatu Kijaji amesema ongezeko la bei ya bidhaa za vyakula kwa mwaka 2021/22 ulichangiwa na upungufu wa uzalishaji wa bidhaa hizo kwa wastani wa tani milioni 1.52 ukilinganisha na tani milioni 18.67 zilizozalishwa mwaka 2020/21. "Uzalishaji kwa mwaka 2021/22 ulikuwa tani milioni 17.15. Bei za bidhaa za chakula hutegemea uzalishaji wa mazao ya mwaka juzi ... huu ndio mwaka uliotutengeneza hali halisi ya upatikanaji wa chakula katika masoko kwa mwaka wa fedha 2022/23," amesema Dk Kijaji mbele ya waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya mwenendo wa bei za bidhaa muhimu nchini leo Julai 25, 2023 jijini Dodoma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live