Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uzalishaji maji wapungua Sikonge

82906 Pic+pump Uzalishaji maji wapungua Sikonge

Wed, 6 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Kuharibika kwa pampu moja na kupungua kwa kina cha maji cha bwawa la Utyatya lililopo mjini Sikonge, kumesababisha kupungua uzalishaji wa maji kwa zaidi ya asilimia 20.

Akitoa taarifa ya hali ya upatikanaji maji mjini Sikonge kwa Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa, mkuu wa wilaya ya Sikonge, Peres Magiri, amesema tatizo hilo limesababisha uzalishaji kuwa lita 390,000 badala ya 600,000 kwa siku.

Amesema mahitaji ya maji kwa mji wa Sikonge ni Lita 1.8milioni kwa siku sawa na Lita 55.9 milioni kwa mwezi.

Magiri amesema mtandao wa maji mjini Sikonge ni asilimia 66 ikiwa na wateja 524, magati 10 na mtandao wa bomba wenye urefu wa km 48.5

Akijibu taarifa ya mkuu wa wilaya, Waziri Mbarawa ameagiza pampu moja ya Nzega ipelekwe Sikonge kuziba pengo la pampu iliyoharibika. "Nzega wanazo pampu mbili na wao baada ya wiki mbili wanatarajia kupata maji ya Ziwa Victoria," amesema.

Waziri Mbarawa amesema serikali itahakikisha wakazi wa Sikonge wanapata maji safi na salama hata kabla ya kupata maji kutoka mradi wa maji ya Ziwa Victoria. Bwawa la Utyatya kwa sasa lina uwezo wa ujazo wa mita za ujazo 900,000 ambapo awali lilikuwa na uwezo wa mita za ujazo 1.6milioni.

Chanzo: mwananchi.co.tz