Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uzalishaji dhahabu Buzwagi washuka

36735 Pic+dhahabu Uzalishaji dhahabu Buzwagi washuka

Wed, 16 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Uzalishaji wa dhahabu katika mgodi wa Buzwagi kwa mwaka 2018 uliporomoka kwa kiwango cha asilimia 51 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Uzalishaji huo ulishuka baada ya upatikanaji wa mawe yenye dhahabu kidogo ndani yake kutokana na uhai wa mgodi huo kuelekeza ukingoni.

Mgodi wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama ulikuwa ni wakia 35,880 ikilinganishwa na wakia 73,604 zilizozalishwa kwa mwaka uliopita (2017).

Taarifa iliyotolewa jana na kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia ya robo ya nne kwa mwaka 2018 imeonyesha mabadiliko ya kupanda na kushuka kwa uzalishaji wa dhahabu katika migodi yake mitatu ya Buzwagi, North Mara na Bulyanhulu.

Ofisa mtendaji mkuu wa Acacia, Peter Geleta alisema katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, kampuni hiyo imeingiza mapato ya dola za Marekani 88 milioni sawa na Sh19.3 bilioni.

“Ninayo furaha kuwataarifu kuwa tumefanikiwa kupata wakia 130,581 ya dhahabu kwa robo ya nne ya mwaka iliyotupatia jumla ya wakia 521,980 za dhahabu. Mafanikio hayo yamekidhi malengo ya uzalishaji yaliyokadiriwa kufikia wakia kati ya 435,000 hadi 475,000,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wakia 521,980 zilizopatikana kipindi hicho ni pungufu ya asilimia 32 ya zilizozalishwa mwaka 2017 kutokana na sababu ya kipindi cha uzalishaji mdogo wa mgodi wa Bulyanhulu.

Sababu nyingine ni mrundikano wa mawe yasiyochenjuliwa.

Kuhusu mgodi wa North Mara, kiwango cha uzalishaji kiliongezeka kwa asilimia 17 (84,079 wakia) ikilinganishwa na wakia 72,018 zilizopatikana mwaka uliopita baada ya kupatikana kwa mawe yenye dhahabu nyingi ndani yake katika eneo la Mashariki mwa Nyabirama.

Kwa upande wa mgodi wa Bulyanhulu, ilisema ulizalisha wakia 10,622 za dhahabu, kiwango ambacho kilikuwa juu ya wakia 2,855 zilizopatikana mwaka uliopita kutokana na athari iliyotokana na hali ya ukame iliyokuwa katika wilaya ya Kahama.



Chanzo: mwananchi.co.tz