Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uzalishaji asali wawekewa mikakati

805adb512d024adbd0accf072537d593 Uzalishaji asali wawekewa mikakati

Tue, 13 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BODI ya Kilimo ya Rwanda (RAB) inaangalia uwezekano wa kuanzisha ushirikiano na Mamlaka ya Maji na Misitu Rwanda ili kutumia misitu kuzalisha asali safi kwa kiwango kikubwa na kuwawezesha vijana kujishughulisha na zao hilo.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Utafiti wa Wanyama na Teknolojia katika Bodi ya Kilimo ya Rwanda, Solange Uwituze alisema hayo wakati akijibu maswali ya vijana wanaofanya kazi za kilimo na biashara hasa uzalishaji asali.

Alisema changamoto inayokabili maamuzi hayo ya bodi ya RAB ni uelewa mdogo wa jamii kuhusu ufugaji wa nyuki na upatikanaji wa nafasi ya ufugaji wa nyuki.

Alisema upatikanaji wa wataalamu wa nyuki ni changamoto nyingine inayokabili sekta hiyo.

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Kilimo, uzalishaji wa asali umepungua kwa kiwango kikubwa kutoka tani 5,000 mwaka 2016 hadi tani 3,500 mwaka 2017.

Kutokana na hali hiyo, wizara hiyo imeweka mikakati ya kupandisha uzalishaji hadi kufikia malengo ya uzalishaji ambayo ni tani 9,000 kufikia mwaka 2024.

Kiasi cha asali inayowezakuzalishwa kitaifa kwa sasa ni tani 4,500, wakati mahitaji ya nchi ni tani 16,800.

Idadi ya mizinga ya kisasa nchini Rwanda inakadiriwa kuwa zaidi ya 83,000, lakini inasemekana kati ya mizinga hiyo ni asilimia 45 tu ndio inafanyakazi na kuzalisha.

Chanzo: www.habarileo.co.tz