Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uzalishaji Konyagi wapaa yashika namba mbili

Clear Bar Top Closures 1200x800.jpeg Uzalishaji Konyagi wapaa yashika namba mbili

Thu, 13 Jun 2024 Chanzo: Mwananchi

Konyagi imetajwa kuwa bidhaa ya pili iliyoongeza uzalishaji wake ikiwa na asilimia 38 ikilinganishwa na bidhaa nyingine nchini katika mwaka 2023.

Konyagi inashika namba mbili baada ya kuongeza uzalishaji kwa asilimia 37.95 ndani ya mwaka mmoja ikiwa imetanguliwa na dawa za pareto ambayo inashika namba moja kwa kuongeza uzalishaji kwa asilimia 87.

Kwa mujibu wa Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Tanzania 2023 ambacho kimetolewa leo Juni 13, 2024, bidhaa tano za viwandani zimetajwa kuongeza uzalishaji wake kwa kiasi kikubwa huku nyingine zikipoteza uzalishaji.

Uzalishaji ulioshuhudiwa katika baadhi ya bidhaa umechochea kukuza thamani ya bidhaa zilizozalishwa viwandani hadi kufikia Sh26.438 trilioni mwaka 2023 kutoka Sh25.034 trilioni mwaka 2023.

“Kukua huku kuliakisiwa na kukua kwa uzalishaji wa dawa za pareto kwa asilimia 87, Konyagi asilimia 38.0, nyavu za uvuvi asilimia 31.0, unga wa ngano asilimia 22.6 na rangi kwa asilimia 17.8,” imeelezwa.

Taarifa hiyo iliyowasilishwa na Waziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo Bungeni pia inaeleza kuwa uzalishaji wa dawa za pareto uliongezeka hadi kufikia tani 325 kutoka tani 173 mwaka 2022.

Konyagi uzalishaji ulifikia lita milioni 31.024 mwaka 2023 kutoka lita milioni 22.489 mwaka 2022, nyavu za uvuvi uzalishaji ulifikia tani 604 kutoka tani 461 mtawaliwa.

Chanzo: Mwananchi