Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwekezaji wa Diaspora waongezeka

Uchumi Kupanda Uwekezaji wa Diaspora waongezeka

Tue, 30 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwamko wa Diaspora kutuma fedha (remittances), na kuwekeza katika sekta za kiuchumi na kijamii hapa nchini umeendelea kuongezeka.

Katika kipindi cha mwezi Januari hadi Desemba 2022 Diaspora waliwekeza takriban shilingi bilioni 4.4 katika ununuzi wa nyumba na viwanja kupitia Shirika la Nyumba la Taifa NHC.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Stergomena Tax amesema hayo wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2023/2024 bungeni mjini Dodoma leo (Mei 30, 2023).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live