Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwekezaji kidijitali na siri ya kasi uchumi wa buluu

Buluu Pic Kidigitali Uwekezaji kidijitali na siri ya kasi uchumi wa buluu

Thu, 27 Oct 2022 Chanzo: mwanachidigital

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi anaendelea na mikakati yake ya kukuza uchumi wa visiwa hivyo, huku ufunguaji wa njia za uchumi hasa wa buluu ukipewa nafasi kubwa ya kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi.

Hata hivyo, matumizi ta teknolojia ya kisasa yanatajwa kama nyenzo muhimu kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) katika kufikia mkakati huo kwani, itasaidia kurahisisha utekelezaji wa shughuli za maendelea na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa kodi.

Hayo yamebainika wakati wa Kongamano la Kitaifa la Sita la Tehama (TAIC 2022), ambalo limefunguliwa na Dk Mwinyi aliyeahidi kuwa SMZ itatumia nguvu ya uwekezaji wa kidijitali kuchangia kasi ya ukuaji wa uchumi wa buluu.

Kongamano hilo ambalo limehudhuriwa na mawaziri, wakurugenzi wa taasisi mbalimbali na wadau wa maendeleo zikiwemo taasisi za fedha.

Akizungumza wakati akiwasilisha mada katika kongamano hilo, Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa NMB, Benedicto Baragomwa, amesema banki hiyo imekuwa mdau mkubwa katika harakati za kukuza uchumi wa buluu visiwani hapa.

Amesema kuwa kupitia NMB, Serikali na taasisi zake zimekuwa zikinufaika na uwekezaji wa kidijitali wa benki hiyo kwenye sekta mbalimbali hivyo, kuchochea mabadiliko.

Amezitaja baadhi ya kazi ambazo wamekuwa wakishirikiana na SMZ ni pamoja na ushirikiano wao na Umoja wa Kampuni za Kutoa Huduma za Utalii Zanzibar (ZATO) ambao umehusisha matumizi ya kadi maalumu ya malipo kabla (NMB, ZATO Prepaid Card) na ule wa Wakala wa Serikali Mtandao (NMB e-government Zanzibar) ambao unahusisha ulipaji malipo ya Serikali kupitia mifumo ya benki hiyo.

"Kupitia NMB e'Government Zanzibar tumewezesha ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Malipo Kidijitali 'One Stop Center' cha Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC), ambako malipo hupitia 'control number' moja hivyo, kurahisisha makusanyo na kukuza pato la Serikali inayochochea sera ya Uchumi wa Buluu," amesema Baragomwa.

Chanzo: mwanachidigital