Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwazi na uwajibikaji sekta ya uziduaji waingiza dola bilioni 3.51

Edede43134e15ffdec16793e93e34f19 Uwazi na uwajibikaji sekta ya uziduaji waingiza dola bilioni 3.51

Sun, 17 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MWENYEKITI wa Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Raslimali za Madini,Mafuta na Gesi Asilia (TEITI), Ludovick Utouh ameeleza uwazi na uwajibikaji ulivyoleta mafanikio makubwa katika sekta ya madini.

Alieleza hayo kwenye kikao ambacho TEITI ilikutana na wadau kuhamasisha matumizi ya takwimu katika sekta ya madini kwa kufuata misingi ya uwazi na uwajibikaji kilichofanyika jijini Mwanza.

Utouh alisema uwazi na uwajibikaji umewezesha kampuni za uchimbaji na utafiti wa madini, mafuta na gesi asilia kukusanya zaidi ya dola bilioni 3.51. katika kipindi cha mwaka 2017/18.

Katika kikao hicho kilichofanyika mjini Mwanza, Utouh alisema uwazi na uwajibikaji pia umewezesha kuanzishwa kwa masoko ya madini na ujenzi wa ukuta wa Mirerani na hivyo kuleta ufanisi katika sekta ya madini na kuwezesha kukuza pato la taifa.

Naibu Waziri wa Madini, Profesa Shukurani Manya alisema serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli ina dhamira ya dhati ya kuona kuwa sekta ya madini inafanyiwa mabadiliko yatakayo wezesha watanzania wote kushiriki katika usimamizi wa raslimali hiyo ya taifa.

Alishukuru kuwapo kwa utaratibu wa kutolewa kwa ripoti za madini kwani unasaidia wananchi kufahamu kwa uhakika aina na kiasi cha kodi zinazolipwa na kampuni kwa serikali yao, ikiwa ni pamoja na gharama za uwekezaji na uzalishaji wake.

“Taarifa hizi zinawezesha wananchi na serikali kufahamu mapato kwa sekta hiyo, kodi na tozo zinazosamehewa, kutolipwa na kampuni, kulinganisha takwimu za uzalishaji madini, gesi asilia na mafuta,” alisema Manya.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira na Usalama Migodini (SHIREMA) mkoani Shinyanga, Peter Yusuph alishukuru kuwepo kwa mazingira na uwazi katika sekta ya madini akisema, umewawezesha kuelewana na taasisi za madini wa namna bora ya kugawana mapato.

Alishukuru kuanzishwa kwa TEITI kwani imewezesha kuwapo kwa mazingira ya majadiliano yenye tija baina ya kampuni za madini, wananchi na serikali, yenye mazingira ya kunufaika kwa pande zote.

Chanzo: habarileo.co.tz