Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwanja waandaliwa kupokea Bombadier

77338 Uwanja+pic

Thu, 26 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tanga. Serikali imeeleza faida itakayopatikana ukarabati mkubwa wa uwanja wa ndege wa Tanga utakapokamilika, ni kuwa na uwezo wa kuruhsu kutua ndege kubwa aina ya Bombadier.

Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) mkoa wa Tanga, Alfread Ndumbaro alitoa taarifa hiyo jana kwenye kikao cha bodi ya barabara.

Ndumbaro alisema ujenzi wa uwanja huo utakapokamilika utawezesha kutua ndege aina ya ATR72 mbili kwa wakati mmoja, Cessna 206-210 tano kwa wakati mmoja.

Alisema hadi sasa hatua ya utekelezaji mradi huo ni kuwa mhandisi mshauri tayari amekamilisha na kuwasilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na kwamba, fidia zimelipwa kwa waathirika 24.

Meneja huyo alisema katika mwaka wa fedha wa 2019/20, Sh6.8 milioni zimepangwa kwa ajili ya utekelezaji mradi huo ambao hata hivyo hakueleza hadi kukamilika utagharimu kiasi gani cha fedha.

Uwanja wa ndege Tanga mjini ni miongoni mwa viwanja vitatu vilivyoteuliwa katika mpango wa kufanyiwa ukarabati mkubwa.

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz