Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwanja wa ndege KIA kuwekewa taa za kisasa

Kilimanjaro Airport Terminal Building Uwanja wa ndege KIA kuwekewa taa za kisasa

Sat, 9 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hai. Mamlaka ya viwanja vya ndege nchini (TAA), imesema mwanzoni wa mwaka 2024, itaanza kuboresha miundombinu ya uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa kuweka taa za kisasa za kuongezea ndege, ili kuondoa changamoto ambayo imekuwepo ya kuzimika kwa taa hizo.

Hayo yamesemwa leo Desemba 8, 2023 na Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Musa Mburah wakati wa ufunguzi wa wiki ya utamaduni wa usalama wa anga, ambayo imefanyika kiwanjani hapo.

Amesema lengo la kuboresha miundombinu hiyo ni kuhakikisha wanaimarisha usalama katika viwanja vya ndege hapa nchini, ambapo tayari wamenunua vifaa vya kisasa vya ulinzi na usalama zikiwemo mashine na viwezeshi ili ndege ziweze kutua kwa usalama zaidi.

"Maelekezo ya Serikali tayari yameshakuja kwetu na mwakani mwanzoni kabisa tutaanza mchakato wa manunuzi ili tupate mkandarasi aweke taa mpya katika uwanja wetu wa KIA, uwanja huu ni wa kimkakati hatuwezi kuuacha upate changamoto ikiwemo taa za kuongozea ndege," amesema.

Mbura amesema kwa sasa ipo miradi mbalimbali inayoendelea kwenye viwanja vya ndege hapa nchini, lengo ikiwa ni kuimarisha usalama wa usafiri wa anga.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema wataendelea kuhakikisha usafiri wa anga unakuwa salama.

"Niwaambie tu wananchi viwanja vyetu ni salama, usalama wa usafiri wa anga uko imara na ndio maana tulipofanyiwa ukaguzi na shirika la anga duniani tulipata asilimia 86.9, Tanzania ikiwa ni nchi ya nne barani Afrika kwa ubora wa viwango vya usalama.

"Niipongeze Serikali na mamlaka ya viwanja vya ndege kwa jitihada kubwa wanazofanya za kuboresha miundombinu ya viwanja vyetu vya ndege, tumeshuhudia sasa hivi uwanja wetu wa Dodoma wakati wowote wa usiku ndege inaweza ikatua kwa sababu wamefunga taa za kisasa, uwanja wa Mtwara nao umefungwa taa, pamoja na maeneo mengine," amesema Mburah.

Akizungumzia ufunguzi wa wiki ya utamaduni wa usalama wa anga,Mkurugenzi wa uwanja wa ndege KIA, Clemence Jingu amesema maadhimisho hayo yanayofanyika kwa wiki nzima, yanalenga kutoa elimu ya usalama wa anga kwa wadau wote wanaoutumia uwanja wa KIA.

"Usalama wa anga ni muhimu, hivyo wadau wote wanapata fursa ya kufahamu nini wanatakiwa kufanya ili wawe na mchango mkubwa katika kuendeleza usafiri wa anga, tunafahamu usafiri wa anga una mchango mkubwa katika uchumi hapa nchini,"amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live