Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwanja wa ndege JNIA kufanyiwa maboresho

JNIA UWANJA DSM (600 X 362) Uwanja wa ndege JNIA kufanyiwa maboresho

Wed, 11 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile amesema uongozi wa uwanja wa ndege wa Kimataiafa wa Julius Nyerere (Terminal 2 jengo la abiria) unatarajiwa kufanyiwa maboresho makubwa mwaka 2024, ambayo yatasababisha kufungwa kwa muda kwa uwanja huo.

Kihenzile ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam wakati akiendelea na ziara yake ya siku mbili yenye lengo la kujionea namna shughuli zinavyoendelea katika uwanja huo.

Kihenzile amesema iwapo Wananchi wataona uwanja huo umefungwa wasishtuke, ila wajue kuwa ni maboresho yameanza na utakamilika haraka ili shughuli ziendelee.

Ameongeza kuwa maboresho hayo ni kutokana na juhudi za Serikali za kuuongezea uwanja huo uwezo wa kuhudumia abiria wengi zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live