Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwanja wa Ndege wa Zanzibar watajwa miongoni mwa viwanja bora Afrika

Uwanja Wa Ndege Zanzibar  Bora Uwanja wa Ndege wa Zanzibar watangazwa kuwa moja ya viwanja bora barani Afrika

Fri, 15 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wa visiwani Zanzibar umetunukiwa zawani baada ya kutangazwa kuwa moja ya viwanja bora zaidi vya ndege barani Afrika.

Hayo yametangazwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar, Seif Abdalla Juma ambaye amesema kuwa, tunzo za kila mwaka za Ubora wa Huduma za Viwanja vya Ndege zinazotolewa na Baraza la Viwanja vya Ndege Kimataifa ambayo ni taasisi inayojihusisha na huduma za viwanja vya ndege kwa lengo la kuunganisha utendaji wa sekta hiyo kwa viwango vya kimataifa, zitaongeza idadi ya watalii wanaotembelea visiwa vya Zanzibar.

Amesema hayo mbele ya waandishi wa habari na kuongeza kuwa: "Tunzo hizo zinazingatia ubora wa uwanja wa ndege kulingana na maoni ya abiria yaliyokusanywa kupitia tafiti za kila siku katika maeneo ya kuondoka na kuwasili abiria hao kote ulimwenguni."

Vilevile amesema kuwa, tunzo hizo zinatolewa kwa kuzingatia vielelezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na wafanyakazi waliojitolea zaidi, wepesi zaidi wa safari kwenye uwanja wa ndege, uwanja wa ndege wenye mvuto zaidi na uwanja wa ndege msafi zaidi.

Afisa huyo wa serikali ya Zanzibar ameongeza kuwa, mafanikio hayo yametokana na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya SMZ katika kuvutia uwekezaji mkubwa kwenye sekta hiyo.

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ndio uwanja wa ndege pekee wa kimataifa visiwani Zanzibar.

Watalii wengi wanamiminika visiwani Zanzibar kila mwaka kutokana na vivutio vyake vya kila namna yakiwemo maeneo ya kale na fukwe za kuvutia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live