Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwanja wa Ndege wa Njombe kuboreshwa, kufungua biashara

Atupele Uwanja wa Ndege wa Njombe kuboreshwa, kufungua biashara

Wed, 13 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete amesema Kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bado inatambua umuhimu wa Uwanja wa Ndege uliopo mkoani Njombe katika shughuli mbalimbali za uchumi.

Naibu Waziri Mwakibete amesema hayo alipotembelea Uwanja wa Ndege wa Njombe ambapo amesema kuwa kiwanja hicho ni miongoni mwa Viwanja 59 nchini ambavyo vinatarajiwa kujengwa nchini ambapo amesema kuwa Mkoa wa Njombe umekuwa na vyanzo vingi vya uchumi hivyo kukamilika kwa uwanja huo kutarahisisha kusafirisha mazao kutoka katika Mkoa wa Njombe ambao unasifika kwa Kilimo cha Parachichi.

Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Deodatus Mwanyika ameiomba Serikali kuujenga Uwanja Huo kwa Kiwango Cha Lami kwani Mkoa wa Njombe Umekuwa Ukichangia Pato Kubwa La Taifa.

Awali akisoma Taarifa ya Uwanja Huo Lidya Mwenisongole mbele ya Naibu waziri wa Ujenzi Na Uchukuzi amesema kuwa Wananchi wa Mkoa wa Njombe wamekuwa Wakichangia katika Uharibifu wa Uwanja huo.

Hamiss amiry ni Mkurugenzi wa Viwanja Vya Ndege vya Mikoa amesema kuwa Uwanja wa Ndege wa Njombe unakila sifa za Kufanyiwa maboresho makubwa Ili Kitumike kusafirisha Mazao yatokanayo na Kilimo.

Mkoa wa Njombe Ni Miongoni mwa Mikoa ambayo inasifika kwa Kuzalisha mazao mbalimbali ikiwemo parachichi,Mbao,Chai,pamoja na Matunda mbalimbali Hivyo Kujengwa kwa Uwanja Huu Wananchi wanaamini Utakuwa Chachu ya Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Njombe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live