Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwanja wa Ndege Iringa kuongeza kasi ya ukuaji utalii

Kairuki Kairuki Iringa.png Uwanja wa Ndege Iringa kuongeza kasi ya ukuaji utalii

Tue, 26 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Daud Yassin amesema kukamilika kwa Uwanja wa Ndege wa Iringa na ujenzi wa barabara inayoenda Hifadhi ya Taifa ya Ruaha vitasaidia kuongeza watalii na kukuza uchumi.

Akizungumza katika Maonesho ya Utalii Karibu Kusini, Yassin amesema tayari uwanja wa ndege umeshaanza kujengwa na upo hatua za mwisho huku mkakati wa ujenzi wa barabara ukiendelea.

"Iringa tunahitajj watalii na ujenzi wa miundo mbinu itakuwa kivutio na kichocheo katika kukuza uchumi wa Mkoa huu," amesema Yassin na kuongeza;

"Nimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, fedha zimetoka na uwanja unaendelea kujengwa, hiki ni kichocheo,"

Awali Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego alisema ni mkakati wa mkoa huo kuona utalii unaendelea kutangazwa na kuwatoa hofu wananchi kuhusu miundo mbinu.

"Barabara ya Iringa - Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Iringa - Pawaga, Mafinga - Madibira, Mafinga - Mgololo na nyingine zinajengwa kwa lami. Tuendelee kuutangaza utalii wetu," amesema Dendego.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema kazi kubwa iliyopo kwa sasa ni kutangaza vivutio hivyo ili vijulikane.

"Sisi Mbeya kuna vivutio vingi vyau utalii, kazi yetu kubwa ni kutangaza, tumeanza na tutaendelea," amesema Homera.

Baadhi ya wadau wa Utalii wamesema bila kuwa na miundombinu yenye ubora itakuwa ngumu kwa mikoa hiyo kufanikiwa kwenye Utalii.

"Barabara ya Ruaha imekuwa kikwazo na kwa taarifa hizi za ujenzi wa barabara huo basi Utalii wa Kusini utafunguka. Watalii wengi hawawezi kutumia njia ya sasa ya vumbi," amesema Emeresiana Longi, mdau wa utalii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live