Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwanja mpya wa ndege hifadhi ya Taifa Nyerere kuongeza watalii

Uwanja Wa Ndege = Nyerre Hifadi (600 X 373) Uwanja mpya wa ndege hifadhi ya Taifa Nyerere kuongeza watalii

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ujenzi wa uwanja mpya wa ndege wa Mtemere katika Hifadhi ya Taifa Nyerere wenye urefu wa Kilometa 1.8 unaotekelezwa na Mradi wa Kuendeleza Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW), unatarajiwa kuwa chachu katika kuongeza idadi ya watalii pamoja na kuongeza pato la Taifa kupitia sekta ya Utalii nchini.

Hayo yamebainishwa na Mwakilishi wa Mradi wa REGROW katika Hifadhi ya Taifa Nyerere, Daniel Mathayo ambapo amesema uwanja uliopo sasa una uwezo wa kupokea ndege 12 na kukamilika kwa Ujenzi wa Uwanja mpya utakaokuwa na uwezo wa kupokea kwa wingi ndege kubwa za abiria kutachochea ongezeko la mapato katika hifadhi hiyo.

"Ndege zinazoshuka katika kiwanja cha sasa zina uwezo wa kubeba abiria sio zaidi ya 20, lakini mradi wa REGROW unatekeleza ujenzi wa uwanja mpya wa ndege ambao utakuwa mkubwa wenye uwezo wa kushusha ndege kubwa zenye uwezo wa kubeba abiria wengi zaidi ya 100, kwahiyo tunategemea uwanja huu wa Mtemere utakuwa chachu katika kuongeza idadi ya Watalii na pia kuongeza pato la taifa"-amesema Mathayo.

Kwa upande wake Mhandisi Mshauri wa uwanja wa ndege wa Mtemere Edson Shayo amesema kuwa Mradi huo ulioanza Juni 12, 2023 unatarajiwa kukamilika Agosti 2024 na mpaka sasa mpaka umefikia asilimia 21.7.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live