Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwakilishi wa Africa watia shaka COP28 kufikia malengo

COP2828.jpeg Uwakilishi wa Africa watia shaka COP28 kufikia malengo

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

“Tulitarajia Mfumo thabiti wenye Lengo la Kimataifa la Kukabiliana na Mabadiliko ya tabianchi (Global Goal on Adaptation - GGA) sasa tunakaribia kumaliza mkutano huu, lakini tunasikitishwa hatuoni maendeleo yoyote kwenye jambo hili muhimu” hii ni kauli ya Waziri wa Uchumi wa Kijani na Mazingira wa Zambia,Collins Nzovu.

Zambia ni Wenyekiti wa Uwakilishi wa Bara la Afrika kwenye majadiliano ya mabadiliko ya tabianchi (AGN) alitilia shaka iwapo mkutano huo wa 28 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC-COP28) utafikia malengo.

Katika mkutano huo unaotarajiwa kumaliza kesho Desemba 12, 2023, Nzovu amesema muda unayoyoma na bado hajaona mwelekeo kwenye mambo muhimu matano yanayotarajiwa na nchi za Afrika.

Mwakilishi huyo amesema Afrika ilidhamiria kwamba COP28 ingeleta usawa na haki kwenye makubaliano ya pamoja yaliyolenga kutoa mwelekeo kwenye hatua za kukabliana na mabadiliko ya tabianchi.

Amesema walitegemea mjadala ya kina unaohusu madhara na uharibifu na namna ya kuleta usawa kwenye kuhama kwenye matumizi ya nishati chafu.

“Tulitegemea pia fedha za kakabiliana na hali hii zingetengwa na nchi zilizoendelea zingewajibika kama iliyotarajiwa kwenye mkutano wa Paris (COP21) mwaka 2015”.

Hata hivyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na Mabadiliko ya Tabianchi, Simon Stiell amesema bado nchi zina saa 24 kufanya uamuzi na ameshauri suala hilo lifanyiwe kazi bila kupoteza muda.

”Wawakilishi wana nafasi, hapa Dubai kwa muda wa saa 24 zijazo, ili kuanza ukurasa mpya. Maazimio makubwa ya hali hewa yanamaanisha ajira zaidi, uchumi imara, ukuaji wa uchumi wenye nguvu, uchafuzi mdogo na afya bora” amesema.

Mwakilishi wa AGN Collins Nzovu amesema katika mikutano hii Afrika inachohitaji ni hatua za kusaidia kukabilina na mabadiliko ya tabianchi na uimara wa mfuko wa madhara na uharibifu ambao ulianzishwa COP27.

”Tunaunga mkono juhudi kwenye mfuko huu ambao mwaka huu kwa mara ya kwaza ulipata ahadi nyingi za fedha na mpaka sasa inakadiriwa mfuko una Dola za Marekani 800 milioni (Sh2 trilioni) lakini inatosha? Haitoshi hata kidogo” ameongeza.

Akizungumzia fedha hizo, Mhadhiri Kituo cha Mafunzo ya Mabadiliko ya Tabianchi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Profesa Pius Yanda amesema ni mwanzo mzuri lakini alitilia shaka utekelezaji huku akiweka wazi kuwa kiasi kilichotengwa ni kidogo.

“Weka mfano wa madhara tunayopata Tanzania kwa kuharibika kwa miuondombinu ya madaraja au barabara tunahitaji kiasi gani? Lakini ahadi za fedha mara nyingi huwa hawatekelezi” amesema

Amesema kuwa Tanzania pekee hiyo fedha haitoshi huku akitoa mfano wa ahadi ya $100 bilioni (Sh250 trilioni) ya kila mwaka (tangu 2009) lakini utekelezaji wake haujaonekani.

Naye Profesa wa Uchumi wa Chuo kikuu cha Denison University Afrika Kusini na mwanaharakati mabadiliko ya tabianchi, Fadhel Kaboub, amesema nchi zilizoendelea (Global North) zinadaiwa na nchi za Afrika na zinakataa kulipa deni hilo.

“Ikiwa nakudai Dola bilioni 100, unatakiwa kunilipa. Badala yake, unanipa mkopo wa Dola 10 wenye masharti ya kudhibiti jinsi ninavyotumia fedha zangu. Unanipa Dola 10 nyingine badala ya kuwa na uhuru na misitu yangu unaizuia (biashara ya kaboni)” amesema

Kaboub aliongeza kuwa “Unawekeza Dola 10 nyingine katika umeme jadidifu ambao ni lazima nikuuzie kwa masharti unayotaka wewe. Unawekeza Dola 10 nyingine nikuzalishie bidhaa zenye thamani ya chini na ubora mdogo ili uniuzie mimi”.

“Hakuna kati ya haya yanapaswa kuhesabiwa kama fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Ni madeni yanayotuletea ukoloni mamboleo”.

Katika hatua nyingine mwakilishi wa AGN, Nzovu amesema kwenye mapito ya nishati (kuacha matumizi ya nishati chafuzi) wanahitajikuanzishwa kwa mpango kazi thabiti na wa kina ukijumuishamuisha vipengele, upeo na mbinu ambazo zinatambua njia tofauti za kufikia malengo ya Paris.

Malengo hayo ni kuhakikisha kuzuia hali joto ya dunua inabaki chini ya nyuzi joto 1.5 sentigredi hadi mwaka 2030.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live