Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uvuvi Ziwa Tanganyika kusitishwa kwa miezi mitatu

Ulega Pic Data Uvuvi Ziwa Tanganyika kusitishwa kwa miezi mitatu

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ametangaza mpango wa Serikali wa kupumzisha shughuli za uvuvi katika ziwa Tanganyika kwa miezi mitatu ili kuwezesha samaki kuzaliana na kuongeza tija kwa wavuvi, wanaofanya shughuli zao ziwani humo.

Waziri Ulega ametoa kauli hiyo Januari 9,2024 alipokuwa akizungumza na wadau wa uvuvi kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kigoma, na baadaye kuzungumza na wananchi na wadau wanaofanya shughuli za uvuvi kwenye Mwalo wa Katonga mkoani hapa, Januari 9, 2024.

Akiwa kwenye kikao cha ndani na wadau wa uvuvi Ulega amesema kuwa utekelezaji wa mpango huo utaanza rasmi Mei 15 hadi Agosti 15 mwaka huu, ikiwa ni utekelezaji wa mkataba wa kikanda wa nchi wanachama wa mamlaka ya Ziwa Tanganyika, unaoweka hatua na taratibu za usimamizi endelevu wa shughuli za uvuvi katika ziwa hilo.

"Pamoja na kufunga shughuli za uvuvi katika Ziwa Tanganyika, Serikali imeanza kutekeleza njia mbadala za kuwawezesha wananchi kujiendeleza kiuchumi ikiwemo kukopesha vikundi maboti na vizimba kwa ajili ya miradi ya ufugaji wa samaki.

“Tayari Serikali imetenga Sh200 milioni kupitia Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (Tafiri) kubainisha maeneo yanayofaa kwa ufugaji huo,” amesema.

Ameongeza kuwa pia zimetolewa Sh400 milioni kwa ajili ya kuanzisha kituo cha uzalishaji wa vifaranga vya samaki bora mkoani humo, kwa ajili ya kuwawezesha wafugaji wa samaki kwa njia ya vizimba kuwa na uhakika wa kuvipata wakati wote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live