Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uturuki kujenga kituo cha kuandaa miradi ya EAC Z’bar

Uturuki Kujenga Kituo Cha Kuandaa Miradi Ya EAC Uturuki kujenga kituo cha kuandaa miradi ya EAC Z’bar

Sat, 3 Sep 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Taasisi ya Iyilik dernegi kutoka nchini Uturuki imeeleza kusudio lake la kujenga kituo kikuu cha kuandaa utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo kwa nchi za Afrika Mashariki kisiwani Zanzibar.

Hatua hiyo imeenda sambamba na kuomba eneo la ardhi kwa Serikali ya Zanzibar kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho kisiwani humo.

Hayo yameelezwa na ujumbe wa taasisi hiyo ulioongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Metin Calbay katika mazungumzo yao na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi katika Ikulu ya Taifa hilo leo Jumamosi Septemba 3, 2022.

Metin Calbay amesema taasisi hiyo ina azma ya kujenga kituo kikuu nchini humo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kudumu katika nchi za Afrika Mashariki “tunaiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kupatiwa eneo hilo ili kufanikisha jambo hili.”

Naye Dk Mwinyi ameipongeza taasisi hiyo kwa azma yake ya kuifanya Zanzibar kuwa kitovu cha biashara hukuaakiahidi kutoa eneo hilo na ushirikiano wote utakaohitajika kutumiza matakwa hayo.

“Serikali itatoa kila aina ya ushirikiano kufanikisha azma hiyo ya kuifanya Zanzibar kuwa kituo kikuu kwa miradi yote inayotekelezwa na taasisi hiyo kwa nchi za Afrika Mashariki,” alisema

Eneo hilo, pamoja na mambo mengine, litahusisha ujenzi wa majengo ya shule kuanzia ngazi ya maandalizi hadi Sekondari, chuo cha kilimo na ufundi.

Taasisi hiyo imefanikisha ujenzi wa nyumba na shule  kwa wakimbizi walioko katika maeneo yenye vita nchini Syria pamoja na kusaidia mbuzi milioni tatu wa maziwa kwa nchi 25 Barani Afrika, ikiwa ni hatua  kusaidia familia zenye maisha duni.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz