Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uturuki, Tanzania mambo ni 'mukide mukide'

B12771c885ac72db18a82a7302ce6866 Uturuki, Tanzania mambo ni 'mukide mukide'

Tue, 12 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mehmet Gulluoglu amesisitiza nchi hiyo kuendelea kuimarisha urafiki na Tanzania pamoja na kuboresha program mbalimbali zenye kukuza uchumi.

Alisema hayo jana Dar es Salaam, wakati akitoa misaada ya nyama kwa watu wenye mahitaji maalum wakiwemo wazee, wenye ulemavu wa ngozi na walemavu.

Msaada huo umetolewa kwa ushirikiano wa Taasisi ya Kizilay kwa uratibu wa Taasisi ya Rehema Foundation inayosimamia vituo mbalimbali kwa ajili ya kusaidia makundi hayo maalum.

Balozi Gulluoglu amesema katika kusherehekea sikukuu ya Eid, taasis hizo zimeona ni vyema kuendelea kuimarisha urafiki nchini, huku wakiwakumbuka wananchi wenye mahitaji.

Amesema serikali ya Uturuki imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha uchumi na ipo miradi kadhaa ambayo imekuwa ikitekelezwa nchini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kizilay, Yusuf Ramadhan alisema Watanania ni ndugu zao, hivyo wameshirikiana katika siku hiyo ili kuhakikisha urafiki unaimarishwa na zaidi, walio wengi kufurahia sikukuu ya Eid.

Mratibu wa kazi ya uchinjaji nyama kutoka Rehema Foundation, Hamza Msuya amesema watu zaidi ya 10,000 wamenufaika na msaada huo umetolewa kwa mikoa takriban 11 nchini Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live