Mbunge wa Kinondoni Abbas Tarimba amehoji kama serikali haioni ni wakati sasa wa kuondoa sharti la kukopa kwa vikundi mikopo inayotolewa na Halmashauri.
Mbunge wa Kinondoni Abbas Tarimba amehoji kama serikali haioni ni wakati sasa wa kuondoa sharti la kukopa kwa vikundi mikopo inayotolewa na Halmashauri. Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), Festo Dugange amesema Serikali iliunda timu ya kitaifa kwa lengo la kupitia na kutoa mapendekezo ya namna bora ya kuratibu na kusimamia utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa na kwamba timu hiyo imekalimisha jukumu hilo na kukabidhi taarifa kwa serikali. - “Mheshimiwa Spika, Aidha, serikali inaendelea na uchambuzi na mapitio ya taarifa na pindi itakapokamilisha taarifa rasmi itatolewa kwa umma juu ya utaratibu wa mikopo ya asilimia 10 katika Mamlaka za Serikali za Mitaa,” amesema.