Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utambuzi wa watoa mikopo ya kilimo waanza

3d55af7bc519930b47caf7eb286ad237 Utambuzi wa watoa mikopo ya kilimo waanza

Wed, 31 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kuwa Serikali imeanza mchakato wa kutambua taasisi zote zinazotoa huduma ya mikopo ya pembejeo za kilimo kwa wakulima ili kufahamu riba wanazotoza.

Bashe amesema hayo leo bungeni Jijini Dodoma alipokuwa anajibu swali la Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Aida Khenani lililohoji kwanini Serikali isibadili utaratibu wa mikopo ya pembejeo kwakuwa ule unaotumika sasa unawaumiza wakulima kwa kuwatoza riba kubwa.

“Hatua hii itasaidia kutambua changamoto zilizopo na kuzipatia ufumbuzi ikiwemo kupunguza riba pamoja na kuweka utaratibu wa kumsaidia mkulima katika kurejesha mkopo kulingana na mapato ya mkulima kwa msimu wa kilimo” amesema Bashe.

Katika hatua nyingine Bashe amesema kuwa wamepanga kuhamasisha sekta binafsi kuanzisha vituo vya kukodisha zana za kilimo ili kusogeza karibu upatikanaji wake kwa wakulima.

“Tupo katika mchakato sekta binafsi kutusaidia kukodisha wakulima zana za kilimo katika maeneo ya karibu ya shughuli zao kwakuwa tuna mpango wa kupunguza matumizi ya jembe la mkono kutoka 53% ya sasa hadi kufikia 10% ifikapo mwaka 2025” amesema Bashe.

Chanzo: www.habarileo.co.tz