Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utalii kuzingatia utunzaji wa mazingira

KATIBU MKUU Utalii kuzingatia utunzaji wa mazingira

Sat, 22 Oct 2022 Chanzo: eatv.tv

Serikali imehimiza shughuli za Utalii nchini kuzingatia utunzaji wa mazingira ili vivutio vilivyopo sasa vidumu kwa manufaa ya wakati huu na wakati ujao.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Eliamani Sedoyeka alipotembelea mabanda mbalimbali kwenye maonesho ya sita ya kimataifa ya Kiswahili ambapo amebainisha kuwa Utalii unatakiwa kutunzwa ili kuongeza zaidi mapato yatokanayo. 

Kwa upande wake Afisa Mhifadhi kutoka Wakala wa Huduma za misitu Tanzania TFS Yusuph Tango ameeleza kuwa kwa sasa wao wanaendelea kufanya utalii wa ikolojia, ambao ni rafiki zaidi kwa mazingira.

Nao wadau wa shughili  za Utalii nchini, wamempongeza Samia Sululu Hassan kwa kuifungua nchi hasa kwa shughuli za utalii, wakiahidi kuendelea kujikita zaidi kwenye shughuli utalii kwa manufaa ya taifa letu.

Katika maonesho haya leo, viongozi mbalimbali wamehudhuria, akiwepo Waziri wa Utalii Balozi Dk. Pindi Chana na Naibu Waziri wake Mary Masanja.

Chanzo: eatv.tv