Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utafiti wa madini waendelea kufanyika maeneo mbalimbali

E1d2ee795667cdfd4458d19f129cd9e7 Utafiti wa madini waendelea kufanyika maeneo mbalimbali

Fri, 12 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WIZARA ya Madini kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kwa nyakati tofauti imefanya utafiti wa awali wa madini katika maeneo mbalimbali nchini.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Madini, Profesa Shukrani Manya bungeni Dodoma jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Manyoni Mashariki, Dk Pius Chaya (CCM).

Dk Chaya alitaka kujua seriali ina mpango gani wa kufanya utafiti ili kubaini uwapo wa madini ya aina mbalimbali katika Jimbo la Manyoni Mashariki.

Akijibu, Profesa Manya alisema wizara na taasisi ya GST ilifanya tafiti hizo katika kata za Makuru, Solya, Kintinku na Sasilo wilayani Manyoni.

“Matokeo ya tafiti za awali yalionesha kuna viashiria vya uwapo wa dhahabu na ulanga katika kata ya Makuru na kata ya Solya kuna madini ya urani, thorium na ya ujenzi,” alisema.

Alisema katika kata ya Kintinku walibaini uwapo wa madini ya urani, ambapo katika kata ya Sasilo hakukuwa na viashiria vya uwapo wa madini.

Profesa Manya alisema ili shughuli za uchimbaji zifanyike lazima utafiti wa kina ufanyike kujiridhisha na kiwango cha mashapo iwapo yanaweza kuchimbwa kwa faida au la.

Chanzo: habarileo.co.tz