Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utafiti ugonjwa zao la ndizi wafikia pazuri

Ndizi Ndiziiii Ndiziiii Utafiti ugonjwa zao la ndizi wafikia pazuri

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Utafiti wa kukabiliana na ugonjwa wa ndizi aina ya mshale unaojulikana kama mnyauko wa fuzari uko katika hatua nzuri.

Mtafiti mwandamizi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Dk Mpoki Shemwela amesema hayo alipozungumza na HabariLeo katika maonesho ya mazao mbalimbali kuelekea Kongamano la Chakula mkoani Dar es Salaam lililoanza leo.

Dk Mpoki amesema utafiti huo umefikia katika hatua nzuri kwa kuwa mpaka sasa tayari aina mpya ya mshale imeshapatikana ipo katika majaribio ya awali katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Mbeya.

” Zaidi ya asilimia 90 ya aina hii ya mshale iliyofanyiwa utafiti inafanana na mshale asilia ambao unapendwa na wachaga.

”Una uzaaji wa kutosha, majaribio ya awali pamoja na wakulima waliozionja walizipenda, zina ladha inayofanana na mshale,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live