Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utafiti maeneo yenye petroli wakamilika

Petroliiii Petroliiii Kukamilika (600 X 354) Utafiti maeneo yenye petroli wakamilika

Tue, 10 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MRADI wa kuchukua data za mitetemo za 2D katika kitalu cha Eyasi Wembere umefikia mwisho huku wataalamu wakieleza kuwa na matumaini ya utafiti huo kubainisha na kuainisha maeneo yenye viashiria vya uwepo wa rasimali ya mafuta.

Hayo yamebainika hivi karibuni wakati wa ziara ya ufuatiliaji iliyofanywa na Maafisa wa Mamlaka ya udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) katika eneo la Eyasi Wembere mkoani Singida ambapo mradi huo umekuwa ukitekelezwa.

Akizungumza na maafisa hao Mjiofizikia wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) na Meneja Mradi huo ,Sindi Maduhu alieleza kuwa utafiti huo wa 2D umefanyika katika maeneo yaliyopo katika Wilaya sita zilizo ndani ya Mikoa mitano ambayo ni Singida, Arusha, Tabora, Shinyanga na Simiyu.

Akieleza historia fupi ya utafiti wa mafuta kwenye bonde hilo la Eyasi Wembere Maduhu alieleza kuwa utafiti ulianza mwaka 2015 kwa kuchukua taarifa za kijiofizia (gravity magnetic) ili kubaini ukubwa wa eneo la bonde na kuangalia kina cha miamba tabaka iliyopo katika eneo husika.

Eneo la Eyasi Wembere lina kilometa za mraba 10630, na utafiti huo ulilenga kusoma aina na kina cha miamba ili kubaini uwezekano wa uwepo wa mafuta au gesi asilia katika eneo husika.

Utafiti katika bonde hilo umekuwa ukiendelea kufanyika kwa vipindi tofauti tofauti na kwa kutumia teknolojia mbalimbali ambapo kufikia mwezi Julai 2023 utafiti wa data za mitetemo kwa njia ya 2D ulianza rasmi kwenye eneo hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live